Tor Project haiendeshi wala haina uwezo wa kuggundua mmiliki au eneo la anwani ya onion. Anwani ya onion ni anwani kutoka kwenye onion service. Jina unaloliona linaishia kwenye onion ni mfafanuzi wa onion service. Hujitengeneza jina kiotomatiki ambalo linaweza kuwekwa katika Tor relay au mtumiaji yoyote katika mtandao. Onion Services zimeundwa kuwalinda mtumiaji na mtoa huduma dhidi ya kugundulika wao ni nani na wanatokea wapi. Muundo wa onion services huficha mtumiaji na eneo la tovuti ya onion hata kwetu sisi.

Lakini kumbuka hii haimaanishi kwamba onion services are haziwezi kuathiriwa. Mbinu za kiasili za mapolisi bado zinaufanisi mkubwa dhidi yao, kama vile mahojiano ya kushuku, aina ya uchambuzi wa uandishi, uchambuzi wa kiufundi wa maudhui yenyewe, uendeshaji wa shughuli, uchapaji wa kibodi, na uchunguzi mwingine wa kimwili.

Kama una malalamiko kuhusu nyenzo za unyanyasaji wa watoto, unaweza kuripoti katika Kituo cha Taifa cha makosa na ukandamizaji wa watoto, ambacho hutumika kama kituo cha uratibu wa taifa cha uchunguzi wa ponografia ya watoto: https://www.missingkids.com/. Hatuoni anwani ya ripoti.