Tor inategemea msaada wa watumiaji na wajitoleaji ulimwenguni kote kutusaidia kuboresha programu yetu na rasilimali, kwa hivyo maoni yako ni muhimu sana kwetu (na kwa watumiaji wote wa Tor).

fomu ya mrejesho

wakati Unatutumia maoni au kutoa taarifa kuhusu hitilafu, tafadhali jumuisha na vingine iwezekanavyo:

  • mfumo wa uendeshaji unaotumia
  • Toleo la Tor Browser
  • Kiwango cha ulinzi wa Tor Browser
  • Hatua kwa hatua jinsi ya kupata suala hilo, ili unaweza kulizalisha tena (kwa mfano Nimefungua kivinjari, nikaandika url, nikabofya (i) icon, kisha kivinjari changu kikapotea)
  • skrini yenye tatizo
  • kumbukumbu

namna ya kutufikia

Kuna njia mbalimbali za kuwasiliana nasi,tafadhali chagua ipi itakufaa zaidi.

jukwaa la Tor

Tunashauri kuomba msaada katika Jukwaa laTor. Utahitaji kutengeneza akaunti ili kuwasilisha mada mpya. Kabla hujauliza, tafadhari hakiki miongozo yetu ya majadiliano. Kwasasa, kwa majibu ya mwisho, tafadhali andika kwa kingereza. Ikiwa umepata programu iliyoharibika, tafadhari tumia GitLab.

#### Gitlab

Kwanza, angalia kama tatizo limejulikana. Unaweza kutafuta na kusoma matatizo katika https://gitlab.torproject.org/. Kuunda jambo jipya, tafadhaliomba akaunti mpya kuipata Tor Project's GitLab haraka na tafuta hifadhi sahihi kutoa taarifa ya tatizo. Tunafuatilia matatizo yote yahusianayo na Tor Browser Tor Browser issue tracker. Matatizo yahusianayo na tovuti yetu yanatakiwa kujazwa katika Kinasa matatizo ya tovuti.

Telegram

Ikiwa unahitaji kusanikisha au troubleshooting Tor Browser na Tor Forum ikizuiliwa au kudhibitiwa mahali ilipo, unaweza kutufikia katika Telegram https://t.me/TorProjectSupportBot. Mtaalam wa msaada wa Tor atakusaidia.

whatsApp

Unaweza kuwasiliana na nasi kwa kutuma ujumbe wa maandishi katika namba yetu ya WhatsApp: +447421000612. Huduma hii inapatikana tu kwa ujumbe wa mandishi; video au simu hazijawezeshwa.

signal

Unaweza kupata msaada kwa kutuma ujumbe wa maandishi katika namba yetu ya Signal: +17787431312. Signalni programu ya matumizi ya bure na imelenga ufaaragha kwa watumiaji. Huduma hii inapatikana tu kwa ujumbe wa mandishi; video au simu hazijawezeshwa. Baada ya kutuma ujumbe,watu wetu wa msaada watakusaidia kutatua tatizo.

barua pepe

Tutumie barua pepe kwa [email protected].

Katika kichwa cha habari cha barua pepe yako, tafadhali tujulishe unatoa taarifa ya kitu gani. Namna ambavyo kichwa cha habari cha barua pepe kinakuwa mahususi mfano. "Kushindwa kuunganishwa", "mrejesho katika tovuti", "Mrejesho katika Tor Browser, "Nahitaji bridge"), ndivyo itakavyokuwa rahisi kwetu kuelewa na kufuatilia. Wakati mwingine tunapopokea barua pepe zisizo na kichwa cha habari,huingia katika barua pepe zisizothibitishwa na tunashindwa kuziona.

Kwa majibu ya haraka, tafadhari andika kwa Kiingereza, Kihispania, na/au Kireno ikiwa unaweza. Kama hakuna lugha unayoielewa kati ya hizi, tafadhali andika kwa lugha yoyote unayoweza, lakini jua kwamba muda kidogo kujibu sababu tutahitaji msaada wa kutafsiriwa ili kuelewa.

blog ya kuweka maoni

Unaweza kuacha maoni kwenye chapisho la blogu linalohusiana na suala au mrejesho unayotaka kutolea taarifa. Ikiwa hakuna chapisho katika suala lako, tafadhari wasiliana nasi kwa njia ingine.

IRC

Unaweza kutupata kupitia #tor kwenye OFTC ili kutupatia maoni au kuripoti makosa. Hatujibu mara moja, lakini tunachunguza orodha ya kazi zilizobaki na tutakujibu kadri tunavyoweza.

Jifunze jinsi ya kujiunga katika OFTC servers.

orodha ya barua pepe

Kwa kutoa ripoti masuala au majibu ya kutumia orodha ya barua pepe, tunapendekeza kwamba ufanye hivyo kwa ile inayohusiana na kile ambacho ungependa kuripoti. Saraka iliyokamilika katika orodha yetu ya barua pepe inaweza kupatikana hapa.

Kwa majibu au masuala yanayohusiana na tovuti yetu: ux

Kwa mrejesho na masuala yahusuyo kutumia Tor relay: tor-relays

toa taarifa ya kiusalama

Ikiwa umepata suala la kiusalama, tafadhari tutumie barua pepe [email protected].

Ikiwa unataka kusimba barua pepe yako, unaweza kupata funguo la umma ya OpenPGP kwa anwani hii kutoka keys.openpgp.org. Here is the current fingerprint:

  pub   rsa3072/0x3EF9EF996604DE41 2022-11-15 [SC] [expires: 2024-12-11]
      Key fingerprint = 835B 4E04 F6F7 4211 04C4  751A 3EF9 EF99 6604 DE41
  uid Tor Security Contact <[email protected]>
  sub   rsa3072/0xF59EF1669B798C36 2022-11-15 [E] [expires: 2024-12-11]
      Key fingerprint = A16B 0707 8A47 E0E1 E5B2  8879 F59E F166 9B79 8C36

Ikiwa unapenda kushiriki katika programu yetu ya bug bounty, tafadhari kuwa makini, kuwasilisha suala la usalama katika tovuti ya watu wengine hubeba hatari fulani ambayo hatuwezi kuidhibiti, ndio matokeo tunapendelea kuripoti moja kwa moja.